loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

RC Kunenge atoa maagizo mazito Dawasa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge ameiagiza Idara ya Maji (DAWASA) kukamilisha Mradi wa Maji wa Kisarawe kwenda Pugu, ifikapo Disemba mwaka huu, kama ilivyoagizwa na Rais Dk John Magufuli wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi.

Katika ziara yake ya kukagua mradi huo, Kunenge alisema utasaidia kusambaza maji kwa wakazi wa Kata ya Kinyerezi na mtaa wa Kifuru, sambamba na maeneo ya jirani, ambapo mpaka sasa mradi huo umefikia asilimia 70.

"Niwapongeze sana Dawasa na vitu vyote hivi vinafanyika kwa kutumia fedha za ndani na mradi huu pia umetoa ajira kwa watazania”amesema Kunenge.

“Agizo langu endeleeni na kazi kwa nguvu mliyoanza nayo na ikiwezekana basi tukamilishe mradi huu hata kabla ya wakati tuliopangiwa na rais Magufuli "amesema Rc Kunenge.
Aidha, amewataka wananchi kuhakikisha wanatimiza wajibu kwa kulipa bili (DAWASA) ili fedha hizo ziendelee kusaidia kazi zinazoendeshwa na Idara hiyo.

 

 

 

 

 

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi