loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzania kuongoza Kamati ya Utambulisho UN

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hati za Utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa mwaka 2020/2021. 

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika nafasi ya kuongoza kamati hiyo nyeti ya Umoja wa Mataifa ambayo uteuzi wake ulipendekezwa na Ofisi ya Rais wa Baraka Kuu la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kwa kauli moja na wajumbe wote tisa wa kamati hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wajumbe hao ni Marekani, China, Urusi, Cameroon, Uruguay, Iceland, Papua Guinea na Trinidad na Tobago pamoja na Tanzania.

Akizungumza baada ya uteuzi huo, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika UN, Balozi Profesa Kenedy Gaston alisema uteuzi huo ni muhimu na ni ishara ya namna Tanzania inakubalika katika uso wa jumuiya ya kimataifa kutokana na uongozi thabiti wa Rais John Magufuli halikadhalika sera zake za mambo ya nje.

Balozi Profesa Gaston aliongeza kuwa kwa mara ya kwanza tangu uteuzi huo, Tanzania imeongoza kikao cha kwanza cha kamati hiyo kilichofanyika jijini New York.

 

ASILIMI 80 ya wafanyakazi wa maofisini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi