loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TFF yazikana fedha ‘chafu’

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi kuhusishwa kwa Rais wake Wallace Karia katika malipo yanayodaiwa kusababisha Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kumfungia miaka mitano Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na kuwaonya wanaopotosha.

Ahmad alifungiwa na Fifa kujihusisha na soka kwa miaka mitano kutokana na kukiuka sheria kadhaa za maadili na kupigwa faini ya Dola za Marekani 200,000.

Mapema jana kwenye mitandao kulikuwa na taarifa inayodai kwamba Tanzania na Cape Verse ni miongoni mwa nchi zilizonufaika na mgao wa Ahmad ambapo inadaiwa Dola 20,000 ziliwekwa kwenye akaunti binafsi ya Rais wa TFF.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, Mei 2017 Kamati ya Utendaji ya Caf ilipitisha uamuzi kila mwanachama wake kupatiwa mgawo wa Dola za Marekani 100,000 (zaidi ya Sh milioni 200) ambazo ziligawanywa kwa nchi wanachama.

Dola 80,000 (zaidi ya Sh milioni 100) kwa matumizi ya shughuli za maendeleo ya soka na dola 20,000 (zaidi ya milioni 40) kwa Rais wa Shirikisho husika kwa ajili ya kumsaidia katika majukumu yake ya shughuli za mpira wa miguu kutokana na hawalipwi mishahara.

“Baada ya mgawo wa Caf kuingia kwenye akaunti ya TFF, Rais Karia alielekeza dola 20,000 zitumike kwa shughuli mbalimbali za shirikisho kutokana na changamoto ya kifedha iliyokuwapo. Hakuna fedha ya Caf iliyowahi kuingizwa kwenye akaunti binafsi ya Karia,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema suala hilo walilitolea ufafanuzi tangu Aprili lilipoibuka kwa mara ya kwanza na kusisitiza kuwa fedha tajwa hazikuwahi kulipwa katika akaunti binafsi ya Karia.

“Taarifa ya Kamati ya Maadili ya Fifa ya kumfungia Rais Ahmad haikuzungumza chochote kuhusu dola 20,000 kwenda kwa marais wa wanachama wa Caf, hivyo TFF haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote wanaoendelea kusambaza taarifa za uongo,” alisema.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Junior Lokosa ametua ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi