loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam, Yanga mechi ya kuwania usukani

TIMU ya Azam FC itakuwa mwenyeji wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga katika mchezo utakaochezwa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam leo.

Huu ni mchezo wa kibabe kwa sababu timu zote zina pointi 25, Azam inaongoza ligi kwa tofauti ya mabao ya kushinda, imeshinda mabao 18 na Yanga imeshinda mabao 13, Azam imefungwa mabao matano na Yanga manne.

Katika michezo mbalimbali waliyokutana Azam ameshinda mara nane sawa na Yanga na sare nane kila mmoja. Kwenye mabao Azam imeifunga Yanga mabao 31 na Yanga imefunga mabao 30.

Jana maofisa habari, Thabit Zakaria wa Azam FC na Hassan Bumbuli wa Yanga walitambiana kila mmoja akijinisabu timu yake itamfunga mwenzake, huku Bumbuli akijivunia kutopoteza mchezo wowote ambao Yanga wamecheza mpaka sasa.

“Tumejiandaa vizuri, hatuna majeruhi zaidi ya Mapinduzi Balama hivyo wachezaji akili yao ipo kwenye kupata matokeo mazuri ili dhamira ya kutwaa ubingwa wa 21 iweze kutimia,” alisema Bumbuli.

Thabit Zakaria kwa upande wake alijivunia takwimu za kuwafunga wapinzani wao katika michezo ya hivi karibuni na kusema Yanga kutopoteza mchezo wowote itafika mwisho leo.

 “Kutofungwa mabao mengi haifanyi tusiwafunge au kutopoteza mchezo siyo suala la kwetu, sisi huko tulipita tangu 2014/2015 tulicheza michezo yote bila kufungwa na katwaa ubingwa kwa hiyo haina nafasi tena,” alisema Zakaria.

Alisema timu yake imejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuendeleza ubabe dhidi ya wapinzani wao kwani katika michezo mitano ya mwisho Azam imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja.

Michezo mingine itakayochezwa leo, Ruvu Shooting wataialika Tanzania Prisons, Mwadui dhidi ya Gwambina na Kagera Sugar watacheza na Biashara United.

Katika michezo iliyochezwa jana, Mbeya City iliifunga JKT Tanzania kwa bao 1-0 lililofungwa na Kibua Denis dakika ya 68 na kuifanya City kufikisha pointi 10 sawa na JKT.

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa ya Nigeria, Junior Lokosa ametua ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi