loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yaifuata Plateau United

TIMU ya Simba imeondoka kwenda Nigeria kuifuata Plateau United kwa ajili ya  mchezo wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa keshokutwa Abuja, Nigeria.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara waliondoka jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwenda Nigeria kupitia Ethiopia wakiwa na wachezaji 24.

Simba wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kuanza vibaya michuano hiyo msimu uliopita baada ya kuondolewa katika hatua kama hiyo dhidi ya  UD Songo ya Msumbiji.

Baada ya mchezo huo Simba watarejea nchini kujipanga kwa mchezo wa marudio uliopangwa kufanyika Desemba 4 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar es Salaam.

Kocha wa Simba, Sven Vandernbrock alisema ameandaa kikosi chake kiushindani na hawataingia kwenye mchezo huo kwa historia ya msimu uliopita.

“Soka la Afrika kwa sasa limebadilika, haya ni mashindano makubwa kila timu imejipanga, mwaka jana tulifanya vibaya lakini safari hii nimewaandaa wachezaji kwenda kushindana na kupata ushindi utakaotupa morali kuona tunasonga  hatua inayofuata,” alisema Sven.

Wachezaji walioondoka ni Aishi Manula, Ally Salim, Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohamed Hussein, Erasto Nyoni, Ibrahim Ame, Joash Onyango, Pascal Wawa na Kennedy Juma.

Wengine ni Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Said Ndemla, Rally Bwalya, Hassan Dilunga, Francis Kahata, Clatous Chama, John Bocco, Meddie Kagere, Miraji Athumani, Bernard Morrison, Luis Miquissone na Ibrahim Ajibu.

Wachezaji ambao wamebaki ni Chris Mugalu na Gérson Fraga kwa sababu ni majeruhi, huku David Kameta kukiwa hakuna taarifa yoyote ya kubaki kwake.

BERNARD Morrison ameng’ara baada ya kuifungia timu yake mabao mawili ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi