loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watendaji wamkera Makamu wa Pili wa Rais

MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Abdalla Suleiman amesema hajaridhishwa na utendaji katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume ikiwa ni pamoja na kutokuwepo mashine za kukagua mizigo.

Suleiman alisema hayo wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika uwanja huo kuona utendaji kazi zikiwemo shughuli za ukaguzi wa mizigo na wageni.

“Sijaridhishwa na utendaji wa kazi katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume ambapo mashine za ukaguzi hazifanyi kazi sijui kwa nini''alisema.

Alisema uwanja wa ndege ni sura ya nchi hivyo ulinzi na ukaguzi wa mizigo ya abiria wanaoingia nchini unahitaji kupewa kipaumbele cha kwanza.

Suleiman alisema kitendo cha kutokuwepo mashine za ukaguzi wa mizigo kwa kiasi kikubwa kinakwamisha mikakati ya serikali kuingiza mapato ya nchi.

Aliwataka watendaji wakiwemo wanasheria kuipitia upya mikataba ili kujiridhisha na kuona utaratibu wa mapato.

“Nawataka wanasheria wa mamlaka ya uwanja wa ndege kuhakikisha mnaipitia upya mikataba yote iliyotiwa saini ili kuweza kujiridhisha na kuona kwa kiasi gani maslahi yake kwa taifa ikiwa ni moja ya hatua ya kujiridhisha.”alisema Suleiman.

Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Viwanja vya Ndege vya Zanzibar, Said Ndumbugani alisema mashine hizo kwa sasa zipo chini ya uangalizi wa kampuni iliyofanya kazi ya kuziunganisha.

''Tunakabiliwa na bajeti ndogo ambayo haiwezi kukidhi mahitaji ya kuendesha kituo cha ukaguzi wa mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume''alisema Suleiman.

Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Rahma Kassim Ali aliwataka wafanyakazi wa Uuwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume waongeze ufanisi ili kuongeza tija kazini.

Alisema hajaridhishwa na utoaji wa huduma kwa wageni wakiwemo watalii wanaowasili kwa kuwa wanachukua muda mrefu hadi kukamilisha taratibu za msingi kabla ya kwenda katika hoteli walizofikia.

Aliwataka wafanyakazi wa Idara ya Uhamiaji waongeze kasi ya kutoa huduma kwa watalii wanaoingia ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu za huduma za viza kwa haraka ili kuepusha usumbufu.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi