loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

JPM awateua Dk Shein, Mwakyembe kuongoza vyuo

RAIS John Magufuli amemteua Rais mtaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu kwa vyombo vya habari jana, Dk Shein anachukua nafasi ya Jaji mstaafu Barnabas Samatta kwa kuwa amemaliza muda wake.

Rais Magufuli pia amemteua Dk Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam.

Dk Mwakyembe anachukua nafasi ya Mariam Mwaffisi ambaye pia amemaliza muda wake. Rais Magufuli pia amemteua Gaudentia Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika. Taarifa hiyo ya Ikulu ilisema kuwa uteuzi wa viongozi hao ulianzau jana Novemba 24, 2020.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi