loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

ATCL kupokea ndege nyingine mwezi ujao

NDEGE mpya aina ya Bombardier Dash 8 Q400 inatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa mwezi ujao.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni ya Ndege nchini (ATCL), Josephat Kagirwa, alilieleza gazeti hili jana kuwa ingawa hawajapata tarehe rasmi ya kuwasili kwake, lakini haitazidi mwisho wa mwezi ujao.

Kagirwa alisema hivi sasa wanasubiri taarifa ya mwisho ya kuwasili kwa ndege hiyo itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 78.

Hadi sasa Serikali ya Awamu ya Tano imenunua ndege mpya 11, nane zimewashawasili, moja ni hiyo inayotarajiwa Desemba, mbili zinaendelea kutengenezwa nje ya nchi.

Kagirwa alisema ndege mbili zilizobaki aina ya Airbus A220-300 zenye uwezo wa kubeba abiria 132 zitawasili mwakani ikiwemo moja inayotarajiwa kuwasili katikati ya mwaka na nyingine mwishoni mwa mwakani.

Miongoni mwa ndege mpya ambazo Serikali ya Awamu ya Tano ilizinunua na tayari zipo hapa nchini zikiendelea na safari mbalimbali za ndani na nje ya nchi ni pamoja na Boeing 787-8 Dreamline mbili, Airbus A220-300 mbili na Bombardier Dash 8 Q400 nne.

Katika kuhakikisha ATCL inazidi kuimarika kwa kuwa na ndege za kutosha, Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025, imeahidi kununua ndege nyingine mpya tano ikiwemo moja ya mizigo.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

1 Comments

  • avatar
    David Mwakalebela
    26/11/2020

    Kazi nzuri sana!

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi