Rais Mteule wa Marekani, Joe Biden amesema nchi hiyo imerejea tena wakati anazindua timu yake ya watu sita muhimu watakaokuwa katika serikali yake wakati akisubiri kuapishwa rasmi mwezi Januari mwakani.
Amesema nchi hiyo imerejea katika hali yake kama zamani na ipo tayari kuongoza dunia kwakuwa bado haijakata tamaa katika kutekeleza hilo.
Ikiwa watathibitishwa,Avril Haines atakuwa mkurugenzi wa kwanza mwanamke katika shirika la upelelezi wa taifa na Alejandro Mayorkas kuwa waziri wa kwanza wa Mambo ya Ndani mlatino.
Tayari rais wa taifa hilo, Donald Trump amekubali kuanza kwa mchakato wa kukabidhi madaraka kwa Biden ila ameendelea kukataa kuwa alishindwa na kurejea madai yake ya uwepo wa wizi wa kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Novemba 3.