Kamishana wa Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk Hallan Kijazi amesema hifadhi hiyo haitofanya kazi na askari atakayekwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo.
Dk Kijazi amesema hayo Mkoani Morogoro alipokuwa anafunga mafunzo ya askari 561 wapya wa hifadhi hiyo yenye lengo la kuwajengea uwezo na maarifa ya kiuhifadhi kabla ya kuanza kazi rasmi.
“Hatutasita kusitisha ajira ya askari yeyote atakayebainika kuwa legelege na tabia zake kutoridhisha katika utendaji wake wa kazi,” amesema Dk Kijazi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwengelo amesema suala la kwenda kulinda rasilimali za taifa sio kazi nyepesi kwakuwa kunahitaji ujasiri mkubwa ikiwemo kumtanguliza Mungu mbele.