loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Pamoja na maboresho bado kuna changamoto kuvifikia vituo vya afya

Licha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na serikali katika kuboresha huduma ya afya kwa wananchi bado kuna baadhi ya watu wanashindwa kuvifikia vituo vya afya ili kupata huduma za kitabibu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto, Prof Mabula Nchembe amesema hayo  hii leo wakati akifungua Kongamano la Afya nchini (Tanzania Health Summit) jijiji Dodoma, lenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya afya hasa kipindi hiki ambacho nchi imeingia katika uchumi wa kati.

  Prof Nchembe amewataka washiriki wa kongamano hilo  kuhakikisha wanajadili  namna ya kutoa huduma bora za afya  kwa wananchi ikiwemo kuboresha vifaa na miundombinu katika  hospitali  zote nchini.

"Kupitia kongamano hili  naomba  mjadilii na kutoa mapendekezo ya namna ya kuwasaidia  watu wa hali ya chini hasa wakulima ambao  hawana bima ya afya pamoja na kutozifikia huduma za afya kiurahisi" amesema Prof Nchembe.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi