loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chuo cha Kodi chafikisha wahitimu 5,153

KUHITIMU kwa wanafunzi 389 katika Chuo cha Kodi (ITA), Dar es Salaam mwaka huu kunakifanya chuo hicho kufikisha wahitimu 5,153 wa kozi mbalimbali kuanzia mwaka 2008 hadi sasa.

Mkuu wa chuo hicho kilicho chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Profesa Isaya Jairo, alibainisha hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia mahafali ya 13 ya chuo hicho yanayofanyika kesho.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo.

Profesa Jairo alisema, katika mahafali hayo wahitimu 165 watatunukiwa Cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki (EASFFPC), 18 watatunukiwa Cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM) na 71 watatunukiwa Stashahada ya DCTM.

Tuzo nyingine na idadi ya wahitimu katika mabano kwa mujibu wa Profesa Jairo ni Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (117) na Stashahada ya Uzamili katika Kodi (18). 

Alisema alisema ni pamoja na kutoa mafunzo ya forodha na kodi kwa watu na taasisi mbalimbali, tayari wanafunzi 5,153 wamepata mafunzo na kuhitimu katika kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 hadi 2020.

“Chuo pia kinatoa ushauri na kuwajengea uwezo watumishi wa TRA, Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na mamlaka nyingine za mapato au kodi za Afrika.

“Kwa sasa chuo kinaendelea na mazungumzo ya kuendelea kuijengea uwezo Mamlaka ya Mapato ya Sudan Kusini pamoja na kuendesha mchakato wa kuijengea uwezo Mamlaka ya Mapato ya Komoro katika ukusanyaji wa kodi na tayari wakuu wa mamlaka hizo na ujumbe wao wapo nchini kushiriki mahafali haya na kuhakikishja wanaweka msingi wa makabaliano,” alisema.

ASILIMI 80 ya wafanyakazi wa maofisini ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi