loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tulia ataka wasichana wataje wahadhiri mafataki

NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania Dk Tulia Ackson amewataka wanafunzi wa kike wawataje wahadhiri wanaowaomba rushwa ya ngono.

Tulia alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, kukiwa na kauli mbiu ‘Inaanza na Mimi.'

Tulia alisema wanafunzi kwenye vyuo vikuu wakiwafichua wahadhiri hao matukio ya rushwa ya ngono vyuoni yatapungua na wanafunzi watasoma kwa amani kwa kuwa kuna wanafunzi wanalazimishwa kufeli kwa sababu wanawakatalia rushwa ya ngono wahadhiri.

“Ninapotoa msisitizo kwa wanafunzi wa kike kutovumilia wanaposumbuliwa na wahadhiri kuhusiana na rushwa ya ngono, sina maana ya kuwa hawapo wanafunzi ambao nao ni kero kwa walimu kwa kujirahisisha ili wasaidiwe kufaulu. Hao wanafunzi wa hivyo pia wapo ila ninaona wanafunzi wanaoombwa ndio wamekuwa wengi zaidi na ndiyo maana ninawataka wajitokeze na kuzungumzia suala hili."alisema

Alisema hata wakati alipokuwa mwanafunzi chuo kikuu kulikuwa na walimu ambao walikuwa wakiwasumbua kuwataka rushwa ya ngono lakini walikataa na hatimaye wakafanikiwa kusonga mbele kimaisha.

Alisema ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru) imeonesha kuwa asilimia 50 ya wanafunzi waliohojiwa kutoka Vyuo Vikuu vya Dodoma (Udom) na Dar es Salaam(UDSM) kuhusiana na rushwa za ngono walikiri kuombwa rushwa hiyo au kusikia wenzao wakilalamikia kuombwa.

Dk Tulia aliwataka wahadhiri na wanafunzi kutumia siku hizo 16 za kupinga ukatili kujadiliana ni kwa kiasi gani wanaweza kukabiliana na suala hilo la rushwa za ngono kwa kuwa kama likiachwa linaweza kusababisha kukawa na wahitimu wengi waliopata vyeti kutokana na rushwa za ngono kitu ambacho ni hatari kwa taifa.

Aliwataka wanajamii kwa ujumla kukabiliana na rushwa za ngono katika maeneo yao kwa kuwa inazidi kushamiri na akatoa mfano wa ripoti ya Taasisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) iliyotaja kuwa asilimai 40 ya wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 46 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia.

Pia alibainisha kuwa asilimia 22 miongoni mwa wenye umri huohuo wamefanyishwa ngono bila ya wao kutaka, na kwamba, matukio ambayo alibainisha kuwa serikali imekuwa ikijitahidi kuyakabili na akaitaka jamii iunge mkono juhudi za serikali.

Pia Dk Tulia aliezea kuwa serikali kupitia Jeshi la Polis limeanzisha madawati ya jinsia zaidi ya 240 yanayosaidia kukabiliana na ukatili kwa wanawake na watoto na akatoa mwito kwa Jeshi la Polisi wabuni mbinu zitakazowavutia zaidi wanawake na watoto kutoyaogopa madawati hayo.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Evance Ng'ingo

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi