loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakulima Ruangwa wavuna bil 18/- za korosho

WAKULIMA wa korosho katika Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wameuza kilo  8,189,484 za zao hilo kwenye minada sita katika msimu wa mwaka huu.

Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya Ruangwa Haroun Kihara alisema korosho hizo zenye thamani ya shs 19,571,082,803.80 ziliuzwa kwa nyakati tofauti, na kwamba, baada ya makato ya kisheria wakulima walipewa jumla shs 17,506,677,677.10.

Kihara alilileza HabariLEO ofisini kwake wilayani humo kuwa, mapato yamepungua kwa sababu ya kupungua kwa uzalishaji wa zao hilo katika msimu huu.

Alisema, makisio yalikuwa kukusanya korosho ghafi kilo 12,000,000 badala yake makusanyo yalikuwa kilo 8,000,000 kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa hasa mvua za kiangazi, upepo mkali iliosababisha maua kudondoka au kukauka.

Kihara alisema, kama uzalishaji ungekuwa kama makisio yaliyofanyika na kwa kuwa bei ya juu ilikuwa shs 2,400 wakulima wangepata shs bil 26.4/-.

Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Likunja wilayani Ruangwa Mazoea Selemani alisema, kwenye minada minne wilayani humo wakulima walipata shs 462,250,000.

Alisema kupitia chama hicho tani 215 za korosho ghafi ziliuzwa kwa mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani.

Selemani alisema, malengo msimu huu ilikuwa kukusanya tani 500 za korosho, lakini hayatafikiwa kutokana mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababisha uzalishaji kupungua.

Hata hivyo alisema mpaka msimu unakwisha inawezekana uzalishaji wa korosho ghafi ukafikia tani 300.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Ruangwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi