loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanafunzi UDSM wafanya vizuri fainali za Tehama

WANAFUNZI wa Kitanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamefanikiwa kuwa miongoni mwa vinara wa fainali za shindano la dunia la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) la Huawei lililofanyika kwa njia ya mtandao mwishoni mwa wiki.

Timu ya wanafunzi hao kutoka Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (COICT) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, walifanikiwa kufika hatua hiyo ya mashindano baada ya kuibuka vinara katika mashindano hayo miongoni ya mwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara.

Shindano hilo lililenga kutoa jukwaa kwa vijana wenye vipaji kwenye Tehama kuonesha uwezo wao, kushindana na kuwasiliana, kuhimiza utafiti wa Tehama na kusaidia ukuaji wa mfumo thabiti wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Licha ya kuwa washiriki wapya zaidi wa mashindano hayo tangu walipoanza kushiriki mwaka 2017, wanafunzi wa Kitanzania wamekuwa wakifanya vizuri zaidi katika mashindano hayo. Mwaka 2019, ni timu tano tu za Kiafrika ikiwemo Tanzania zilizofanikiwa kuingia fainali hizo ambapo zilifanikiwa kuvuna tuzo moja kati ya tatu, ikilinganishwa na timu 13 mwaka huu, ambazo zimeshinda medali saba.

Timu ya wanafunzi hao wa Kitanzania iliundwa na wanafunzi Mpoki Mwaisela, Hongo Kelvin, Henry Kihanga, Aghatus Biro, John Lazaro na Elisante Akaro.

Akizungumzia ushindi huo kwa niaba ya wenzake, mwanafunzi Hongo alisema: "Mashindano hayo ya Huawei pamoja na kutujenga kiuwezo, yamekuwa na tija kwetu ikiwemo kutupatia vyeti vya utambuzi kuhusu mafanikio yetu katika taaluma hiyo.’’

Mafanikio ya wanafunzi hao yanatajwa kuwa ni kwa sababu ya kutambuliwa kwa jitihada za nchi za Afrika katika kujenga vipaji vipya kwenye sekta ya Tehama ambao watakuwa kichocheo katika kurejesha ustawi wa bara hili baada ya janga la covid-19.

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, Huawei imesaini makubaliano ya ushirikiano na vyuo vikuu zaidi ya 10 vya Tanzania juu ya kuanzisha Taaluma za Tehama za Huawei. Ushirikiano huu umewezesha washiriki zaidi ya 600 kutoka vyuo vikuu kupata vyeti vya Tehama vya Huawei, ambayo huwafanya wawe washindani bora kwenye ajira zinazohusisha Tehama.

Profesa William Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, aliwasifu wanafunzi hao kwa ushindi wao mkubwa na kuinua uwakilishi wa chuo hicho.

Kwa upande wake, Hou Tao, Makamu wa Rais wa Huawei duniani, aliangazia shauku ya kuvutia ya wanafunzi, ambayo inahitajika sana kwa ujumuishaji wa dijiti wa Afrika katika zama ambazo mvuto wa ujuzi wa mahali pa kazi tayari unabadilika mtandaoni.

Mashindano ya Tehama ya Huawei mwaka huu yalivutia takribani wanafunzi 150,000 kutoka vyuo vikuu zaidi ya 2,000 katika nchi zaidi ya 82.

Wanafunzi 327 kutoka nchi 39 walishiriki fainali hizo zilizofanyika kwa njia ya mtandaoni na kufanya kiwango kuwa kikubwa zaidi kwa miaka yote.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi