Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewaagiza makamanda wa polisi kote nchini kuhakikisha wanafanya operesheni katika maeneo yote yanayokusanya chuma chakavu kwa lengo la kubaini watu wanaohujumu miundombinu ya reli ya mwendokasi ili wachukuliwe hatua za kisheria.
Aidha, Sirro ameutaka uongozi wa ‘TRC’ kuwapatia elimu askari wa jeshi la polisi kutambua nyaraka za miundombinu hiyo jambo litakaloongeza umakini zaidi kwenye ufuatiliaji wa kesi hizo.
Katika hatua nyingine Sirro amewaonya watanzania kuacha tabia ya kuchukua vyuma vya reli kwani kwa kufanya hivyo kutawaingiza kwenye matatizo makubwa.