loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wajasiriamali wakumbushwa kuzingatia maagizo kwa faida yao

WAFANYABIASHARA wa mboga na matunda wametakiwa kutii sheria na maelekezo yanayotolewa na Halmashauri ya jiji la Dodoma ya kuacha kufanya biashara eneo lisilo salama kwao na bidhaa kwenye Stendi ya Daladala ya Sabasaba.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Wanawake wajasiriamali soko la Sabasaba, Anna James.

Alisema kitendo cha kufanya biashara katika maeneo ambayo yanatumiwa na daladala ni kuhatarisha usalama wao na mali zao.

Mwenyekiti huyo alisema hayo alipokuwa akizungumza na wajasiriamali mbele ya Ofisa masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna, baada ya kuwatembelea kuwaelimisha wafanyabiashara hao ambao hufanya shughuli zao za uuzaji wa mboga na matunda kwenye eneo hilo la stendi ya daladala iliyopo Sabasaba jijini Dodoma.

Alisema wafanyabiashara hao hawana sababu za kukaidi maelekezo, sheria na kanuni zilizowekwa na Jiji bali wao wanachopaswa kufanya ni kuunga mkono juhudi hizo zinazofanywa za kuwa na mpangilio mzuri katika uendeshaji wa biashara jijini hapo.

"Akinamama ninawaomba tuiunge mkono Halmashauri yetu ya Jiji la Dodoma kwa hili ambalo lipo kwa ajili ya usalama wetu, tuwe tayari muda wote kutoa ushirikiano kwa vitendo na maelekezo yatakayotolewa ikiwemo hili la kupisha eneo hili la stendi ya Sabasaba ili daladala ziwe zinafanya kazi yake kwa uhuru na uwazi kwenye eneo hili,"alisema.

Ofisa masoko wa Jiji la Dodoma, James Yuna aliwataka wafanyabiashara wa stendi ya Sabasaba wanafanya shughuli zao kwa mpangilio, ili kuepuka mwingiliano kati yao na  waendesha daladala ambao wamekuwa wakiegesha  magari yao.

Alisema kwa kuwa na mpango mzuri watakuwa na uhuru  na biashara zao tofauti na ilivyo kwa  sasa ambapo kuna mwingiliano mkubwa unaoweza kusababisha kutokea ajali kwa upande wao.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi