loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serikali yafufua zao la pamba Kilombero, Ulanga, Malinyi

SERIKALI imesema kutokana na uhitaji mkubwa wa zao la pamba nchini wameamua kuyafufua maeneo yaliyokuwa yakilima kwa wingi zao hilo, zikiwemo wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi mkoani Morogoro.

Akizungumza na wakazi wa wilaya hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba nchini, Marco Mtunga alisema wakazi wa maeneo hayo wanatakiwa kulima zao hilo ili kujiinua kiuchumi na sio kutegemea zao moja la mpunga.

Mtunga alisema zao la pamba siyo geni kwa wakazi wa maeneo hayo na katika kuwahakikishia kuwa serikali imejikita katika zao hilo, wameamua kumtafuta mwekezaji ambaye atajenga kiwanda cha kuchambua pamba kitakachokuwepo katika Kata ya Lupiro wilayani Ulanga.

Mkurugenzi huyo amemtaja mwekezaji huyo mzawa kuwa ni Kampuni ya Upami Agro Business Ltd na ameamua kuweka kiwanda Lupiro kutokana na eneo hilo kuwa katikati ya wilaya zote tatu, hivyo kurahisisha usafirishaji wa pamba tofauti na siku za karibuni zao hilo kusafirishwa hadi mkoani Singida kwa ajili ya soko.

Alibainisha kuwa katika kuwahakikishia upatikanaji wa uhakika wa pembejeo na soko, serikali na mwekezaji watawapatia wakulima pembejeo kwa mkopo na wakati wa uuzwaji ndipo watakapolipa huku suala la soko akisema kuwa ni la uhakika na wananchi watalipwa siku ya mauzo.

Mtunga aliwataka wakulima katika bonde hilo kuwatumia wataalamu katika kilimo hicho ili kupata mazao mengi zaidi na kudai kuwa zao la pamba litamsaidia mkulima kulinda chakula alichovuna kwani zao la pamba lina uhakika wa soko na litakuwa la biashara huku mpunga likiwa zao la chakula.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Upami Agro Business, Vitus Lipagila aliwatoa hofu wakulima wa pamba katika wilaya hizo kuwa pamba yao yote itanunuliwa kwa bei nzuri na kwa wakati na kampuni yake sababu anafahamu kuwa wilaya hizo wakazi wake walikuwa wakulima wakubwa wa zao hilo ila uhakika wa soko na mkazo wa kilimo ndio ulifanya wananchi kuacha kulima zao hilo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Malinyi, Mathayo Maselle ameipongeza serikali kwa kuamua kulifufua zao hilo katika wilaya na kusema kuwa yeye anafahamu kuwa zao la pamba lina utajiri mkubwa na hiyo itakuwa ni fusra kubwa kwao baada ya wakazi wake kutegemea zao la mpunga pekee.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Ulanga

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi