loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtaa wa Berlin wapewa jina la Mtanzania

MADIWANI katika Jiji la Berlin wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara la gavana wa nyakati za ukoloni katika eneo la Afrika Mashariki aliyeshutumiwa kwa mauaji na kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania.

Barabara hiyo iliyopewa jina la Hermann von Wissmann, ambaye alikuwa Gavana katika nchi za Afrika Mashariki sasa itaitwa LucyLameck-Straße. Lucy Lameck alikuwa waziri wa kwanza mwanamke nchini Tanganyika sasa Tanzania pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru wa taifa.

Lameck alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Kijamii na Afya na alifanya kazi kuimarisha nafasi ya mwanamke.

Von Wissman alikuwa gavana wa taifa la Ujerumani Afrika mashariki ambayo kwa sasa ndio mataifa ya Tanzania, Burundi na Rwanda katika mwisho wa karne ya 19 na anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wakazi wengi kwa mujibu wa gazeti la Der Tagesspiegel. Kundi la Berlin Postkolonial, mojawapo ya kundi lililohusika na mabadiliko liliunga mkono hatua ya serikali hiyo ya mtaa.

Katika taarifa lilisema kwamba kampeni hiyo ilizuia kuheshimiwa kwa Von Wissmann na nafasi yake kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi. “Wissmann alikuwa mbaguzi na mhalifu wa kivita.

Lucy Lameck anawakilisha mchango ulioshushwa thamani wa wanawake wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo”, gazeti hilo lilimnukuu akisema mwanaharakati wa Tanzania, Mnyaka Sururu Mboro.

Alizaliwa mnamo 1934 Moshi mjini iliyokuwa Tanganyika ya Kiingereza. Alizaliwa katika familia ya wakulima, akajifunza kazi ya uuguzi kabla ya kuingia katika shughuli za siasa. Baada ya mafunzo ya kazi ya uuguzi mnamo 1950, hakutaka kushiriki katika mfumo wa matibabu wa kikoloni wa Uingereza, na kwa hiyo alianza kufanya kazi ya karani.

Mwaka 1960 aliingia mara ya kwanza katika Bunge la Tanganyika kabla ya kuchaguliwa katika Bunge la Tanzania mnamo 1965.

Anakumbukwa kama kielelezo cha kuigwa, akiwa amefanya kazi katika maisha yake yote kuboresha hali ya wanawake nchini Tanzania.

foto
Mwandishi: BERLIN, Ujerumani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi