loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wahitimu waagizwa kutochagua maeneo ya kutumia taaluma zao

WAHITIMU 5,732 wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (LGTI) mkoani Dodoma wametakiwa kutochagua maeneo ya kuzifanyiakazi taaluma walizosomea.

Akizungumza katika mahafali ya 12 ya Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI), Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Joseph Nyamhanga alisema wahitimu wanaobahatika kupata ajira wanatakiwa kuitikia mwito wa kwenda kufanya kazi mahali popote wasichague kubaki mjini.

"Nawataka wahitimu wote mtakaopangiwa kazi kwenda kusaidia jamii vijijini msikatae kufanya kazi katika maeneo hayo, muige mfano wa kada nyingine kama za afya, kilimo na elimu ambazo watumishi wake wakipewa ajira hata vijijini wanaenda kufanya kazi," alisema.

Katibu Mkuu huyo aliagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuwakumbuka wahitimu wa chuo hicho na kuwapa kipaumbele  zinapotokea nafasi za ajira katika halmashauri zao.

"Napenda kuchukua nafasi hii kutoa mwito kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini kunapokuwa na nafasi za kazi kwenye Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji ni vyema wahitimu wa chuo hiki wakapewa kipaumbele," alisema Nyamuhanga.

Pia alisema wahitimu kutoka chuo cha serikali za mitaa wamebobea katika taaluma ya serikali za mitaa hivyo wapo katika nafasi nzuri ya kuleta maendeleo na ufanisi katika sekta hiyo.

Nyamhanga pia alikitaka chuo hicho kuendelea kutumia utaalamu uliopo kuzijengea uwezo Mamlaka za serikali za mitaa kwa ubunifu na kuendelea kufadhili utafiti kutatua matatizo mbalimbali katika jamii.

Naye mkuu wa chuo hicho , Dk Mpamila Madale alisema kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yao ya kuzijengea uwezo Mamlaka za serikali za mitaa nchini kwa kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi, kufanya tafiti na kutoa ushauri elekezi.

Madale alisema chuo hicho kinachotoa kozi 18 kimekuwa kikitoa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu tangu mwaka juzi kimeanza kutoa shahada ya kwanza na katika msimu huu kinajiandaa kutoa mafunzo kwa madiwani wote walioteuliwa nchini ili kuwapa taaluma na mipaka ya kazi zao.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi