loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

  Out waendesha mafunzo elekezi kwa wanafunzi

KITIVO cha Sanaa na Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (CKHT) kimeendesha mafunzo elekezi kwa wanafunzi wapya na wanaoendelea huku wakuu wa idara wakitoa maelezo ya namna ya usomaji chuoni hapo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo elekezi jana na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa chuo hicho na wanafunzi wapya na wanaoendelea ndani na nje ya Dar es salaam, Mtivo Mshiriki, Dk Emmanuel Mhache aliwakaribisha wanafunzi wanaoanza na wanaoendelea katika Mwaka mpya wa masomo wa 2020/21 huku akitoa baadhi ya maelekezo kuhusu kitivo hicho.

“Ili mwanafunzi ahititimu shahada ya kwanza anapaswa kusoma masomo yenye ujazo wa vipimo kati ya 36 hadi 40 kwa kutegemea matakwa ya kozi husika”, alisema Dk Mhache.

Akizungumzia usomaji na ujifunzaji kwa ngazi ya shahada ya kwanza alisema unafanyika katika mfumo wa elimu huria na masafa.

Ufundishaji na usomaji unafanyika kwa mifumo mchanganyiko ikihusisha kuonana ana kwa ana na kwa kupitia mifumo ya Tehama ya chuo ikiwemo ‘Moodle’ na programu tumizi ya ‘Zoom’, alisema Dk Mhache.

Alisema kila kozi imegawanyika katika maeneo sita ya kimaarifa na yana matini na maudhui ya kujisomea katika mfumo wa maandishi, video na uwasilishaji kwa ufupisho.

“Kila eneo moja la kimaarifa linafundishwa kwa Mwezi mmoja ambapo kwa wiki mbili za mwanzo mwanafunzi anapaswa kujisomea na wiki mbili nyingine ni kwa ajili ya uwasilishaji wa kazi na mazoezi kwa eneo husika”, alisema Dk Mhache.

Mkuu wa Idara ya Uandishi na Msomo ya Habari, Kahenga Dachi aliwakumbusha wanafunzi umuhimu wa kutumia njia za mawasiliano katika kuwasiliana na wahadhiri wa masomo husika au popote watakapohitaji kupata maelekezo zaidi.

Alisema kwa mawasiliano rahisi wanatakiwa kuwa na baruapepe za chuo ambazo watatengenezewa na wataalamu wa Tehama mikoa walipo na kwamba wategemee kupata mrejesho kwa muda usiopungua siku tatu.

“Ikiwa hutapata mrejesho ndani ya siku tatu unaweza kutuma baruapepe ya kukumbusha na baada yah apo unaweza kutumia njia ya mawasiliano nyingine ambayo ni kupiga simu”, alisema Dachi.

Mkuu wa Idara ya Utalii na Ukarimu chuoni hapo, Dk Halima Kilungu aliwakumbusha wanafunzi wapya na wanaoendelea kuwa CKHT hakina madarasa ya ana kwa ana kama vyuo vingine kutokana na mfumo wake katika utoaji elimu.

“Huu ni utofauti na upekee ambao hautakufanya uache kazi yako au shughuli yako kwa ajili ya kusoma”, alisema Dkt.Kilungu.

Mkuu wa idara ya Historia, Falsafa na Ukutubi, Dk Lilian Isowe aliwataka wanafunzi wapya na wanaoendelea kuwasiliana na vituo vya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania vilivyopo nchi nzima ikiwa watapata changamoto yoyote katika mchakato wa kujisomea.

 

 

ASILIMI 80 ya wafanyakazi wa maofisini ...

foto
Mwandishi: Vincent Mpepo, OUT

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi