loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

7 mbaroni kwa kukutwa na vyuma vya reli

 

JESHI la Polisi nchini limewafikisha mahakamani watu saba wakituhumiwa uhujumu uchumi kwa kukutwa wakisafirisha vyuma chakavu vikiwemo vyuma vilivyoibiwa kutoka kwenye miundombinu ya reli.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Richard Boaz miongoni mwa watuhumiwa waliofikishwa mahakamani ni pamoja na mawakala na wafanyabiashara wenye viwanda vya kuchakata vyuma chakavu.

Boaz alisema kuwa serikali inatumia fedha nyingi za nchi kwa kuimarisha miundombinu ikiwemo ya reli lakini baadhi ya watu wasio wema na wenye uchu wa mali wamekuwa wakihujumu jitihada hizo za serikali.

"Hali hii haikubaliki wala haivumiliki kwani jeshi la polisi na vyombo vingine vimejidhatiti vyema kuhakikisha miundombinu hii inalindwa kwa nguvu zote," alisema Boaz.

Alitoa onyo kwa watu wenye malengo ya kuhujumu jitihada za serikali waache mara moja kwani hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na wananchi wema wawe walinzi wa miundombinu hiyo.

"Novemba 24, mwaka huu tulitoa taarifa ya kukamatwa watuhumiwa watatu wakiwa wanasafirisha vyuma chakavu vikiwemo vyuma vilivyoibiwa kutoka kwenye miunombinu ya reli zetu na baadaye wakakamatwa watuhumiwa wengine wanne ambao kwa pamoja walipandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazowakabili,"alisema Boaz.

Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakama ya Hakimu mkazi Kibaha ni Shakanyi Gambarata, Shadrack Makulu, Halid Juma, Florence Angelo, Satyam Gupta, Luo Xingqui na Rospick Kimaro

Walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha mbele ya Hakimu Joyce Mushi na mbele ya wakili wa Serikali Mwandamizi , Apimaki Mabrouk na Aurelia Makundi wakili wa serikali.

 

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: John Gagarini, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi