loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

DC ataka watumishi wote kuhamia vituo vya kazi

MKUU wa wilaya ya Rorya Simon Odunga ameagiza watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya hiyo wanaokaa mbali kuhamia katika vituo vyao kazi ndani ya siku 90.

Kiongozi huyo alisema tangu kuanzishwa Halmashauri hiyo baadhi ya watumishi wameendelea kuishi nje ya wilaya hiyo wakilazimika kusafiri umbali mrefu kila siku kufika katika vituo vyao vya kazi.

Alitoa agizo hilo wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika utaratibu wa kushirikisha Idara za Halmashauri, ofisi ya mbunge wa jimbo la Rorya Jaffari Chege na ofisi ya DC.

"Nimetembelea kata na vijiji karibu vyote wilayani hapa na kubaini changamoto ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufika katika huduma za jamii hasa makao makuu ya wilaya badala ya huduma hizo kuwafuata walipo,” alisema.

Alisema lengo la serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma za msingi kama vile afya, elimu na maji kwa wakati huku nidhamu ya watumishi wa umma ikipewa kipaumbele.

Alishangazwa na uamuzi wa baadhi ya watumishi wa Wilaya hiyo kuendelea kuishi wilaya jirani ya Tarime zaidi ya kilometa 30 na hivyo baadhi yao kuchelewa kazini bila sababu za msingi.

Katiba hatua nyingine alihimiza Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kuwekewa katika ujenzi wa nyumba bora wilayani humo kutokana na upungufu mkubwa uliopo baada ya kuanzishwa wilaya hiyo iliyomegwa kutoka Tarime.

Mbunge wa jimbo hilo, Jaffari Chege alisema tayari ofisi yake iliwasilisha mapendekezo katika ofisi ya mkurugenzi wa NHC juu ya kuwekeza katika jimbo hilo ambalo idadi ya wakazi wake iliongezeka baada ya kuanzishwa wilaya ya Rorya.

"Ofisi yangu iliwasiliana na Mkurugenzi wa Shirika la nyumba la Taifa kuelezea umuhimu wa kuwekeza katika sekta ya majengo bora kutokana na mahitaji makubwa yaliyopo jimboni hapa,” alisema Chege.

Alisema watumishi wote wa umma bila kujali vyeo wahakikishe wanaepuka kufanyakazi kwa mazoea na kujenga utaratibu wa kutembelea wananchi maeneo yao kusikiliza n.a. kutatua kero zao mahali walipo.

 

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi