loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

UDSM yaagiza tafiti zenye tija

 

CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeasa wanafunzi kufanya tafiti zenye tija zitakazokuwa na mchango mkukwa katika kutatua na kupunguza changamoto za Watanzania walioko mjini na vijijini.

Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye alisema hayo wakati akiwakaribisha wanafunzi waliojiunga kusoma shahada ya uzamili na uzamivu chuoni hapo.

Profesa Anangisye alisema wanafunzi hao wa shahada ya pili na ya tatu sehemu kubwa ya masomo yao inajikita kwenye kufanya utafiti tofauti na wale wanaosoma shahada ya awali.

“Wao shule yao ni utafiti. Na utafiti ambao unalenga kushughulika na changamoto ambaxzo zinawakilisha watanzania,” alisema na kuongeza kuwa ndio maana chuo hicho kina Naibu Makamu Mkuu wa chuo anayeshughulika na utafiti,” alisema.

Alisema kwa zile tafiti ambazo tayari zimefanyika chuoni hapo ambazo zinalenga kutatua matatizo ya watanzania wanazikusanya na kuandaa takwimu yake.

“Utafiti unafanyika kwenye uhandisi, uchumu, elimu na kwenye elimu kwa mfano watu wamefanya utafiti wa kupunguza utoro shuleni. Matokeo yake yamekuwa yakisaidia taasisi zinazohusika kutatua tatizo hilo,” alisema.

Alitoa wito kwa wanafunzi hao waliojiunga kwenye mwaka wa masomo 2020/21 wajue wamefuata nini chuoni hapo kwani shahada ya uzamili na uzamivu anayehusika zaidi ni mwanafunzi hivyo ni wajibu wake kujua ameenda kufanya nini chuoni hapo.

“Kuna maktaba nzuri na miundombinu ya  kuwawezesha wanafunzi hao kutimiza ndoto zao,” alisema.

Kwa upande wake, Aidan Nzoa anayesoma shahada ya uzamili ya usimamizi na uongozi katika elimu alisema utafiti wake atakaoufanya utajikita kwenye sera ya elimu hususani kwenye mitaala ya elimu kwa ni kimsingi hiyo ndiyo inafanya elimu iwe bora.

Alisema elimu bora ni ile inayoendana na mazingira kulingana na wakati uliopo.

“Mitaala iliyopo sasa ni kiasi gani inakidhi mahitaji ya wanafunzi na jamii iliyopo sasa na mbeleni. Mtaala ili uwe na tija lazima uendane na mazingira yaliyopo,” alisema.

Kwa upande wake, Faustine Christopher anayesoma Kemia chuoni hapo alisema kwenye utafiti wake atajikita katika mazingira maana kipindi hiki ni cha uchumi wa kati hivyo viwanda vinaongezeka kwa namna moja au nyingine kunakuwepo na uchafuzi wa mazingira.

Alisema kuna haja ya kudhibiti uchafu unaotoka viwandani ili mazingira yawe safi.

WAZIRI wa Nishati na Madini, Dk ...

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi