loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wadau waalikwa kutatua changamoto za Mzumbe

 

KATIKA kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kushirikisha sekta binafsi kwenye uwekezaji wa shughuli za maendeleo nchini, Uongozi wa Chuo kikuu cha Mzumbe umewaalika wadau mbalimbali kushiriki katika utatuzi wa changamoto za chuo hicho.

Hayo yalibainishwa na Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka alipokua akitoa hotuba katika mahafali ya 19 ya Chuo hicho Ndaki ya Mbeya yaliyofanyika jana jijini hapa.

Profesa Kusiluka alisema Chuo kikuu Mzumbe katika Ndaki zake za Mbeya na Dar es Salaam zinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa madarasa, hosteli na miundombinu mbalimbali hivyo ili kutatua inabidi sekta binafsi zishirikishwe.

Alisema hivi sasa tayari Chuo hicho kimetenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji hivyo wadau kupitia sekta binafsi wanakaribishwa kutumia fursa hiyo ambayo mbali na kunufaika nazo pia Chuo kitakua kimetatua changamoto zake.

Alitolea mfano katika Ndaki ya Mbeya, Chuo hicho kimetenga eneo la Iwambi lililopo jijini hapa kwa ajili ya wadau kuwekeza kujenga miundombinu ambayo itakisaidia Chuo kujiendesha.

"Serikali imetengeneza utaratibu wa kuhakikisha sekta binafsi zinashiriki katika kuleta maendeleo kwa kutenga maeneo na kujenga mazingira rafiki ya uwekezaji hivyo kwa niaba ya Chuo kikuu Mzumbe nawakaribisha wote wenye nia" alisema Profesa Kusiluka.

Aidha, alimpongeza Rais John Magufuli kwa kusaidia zaidi ya Sh bilioni 15 kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa miundombinu ya Chuo hicho na kuwataka wanafunzi na watumishi wanaotumia miundombinu hiyo kuitunza.

Awali, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo kikuu Mzumbe, Profesa Mathew Luhanga alimpongeza Mkuu wa Chuo hicho Jaji mkuu mstaafu, Barnabas Samatta kwa kukitumikia kwa muda mrefu uliowezesha kupata mafanikio makubwa.

Alisema katika kipindi cha uongozi wake wa miaka 12 Chuo kimepata mafanikio makubwa ikiwemo kukua kwa taaluma na upatiokanaji wa miundombinu bora iliyowezesha kupanda hadhi kwa ndaki zake.

Alisema Ndaki ya Mbeya ilianzishwa mwaka 2006 ikiwa na wanafunzi 405 waliosomea programu mbili tu lakini hadi sasa katika mwaka wa masomo 2019/2020 jumla ya wanafunzi 3786 walisajili na waliohitimu ni 1229 ambapo wanawake ni  659 sawa na asilimia 53.6 huku wanaume wakiwa 570 sawa na asilimia 46.4 katika programu 12.

Pia, Mwenyekiti huyo alimshukuru Rais Magufuli kwa kumteua Dk. Shein Rais Mstaafu wa Zanzibar kuwa Mkuu wa Chuo hicho akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu Samatta anayemaliza muda wake.

Alisema Chuo kipo tayari kumpokea na kumuonesha ushirikiano mkubwa kama walivyofanya kazi na Mkuu wa Chuo anayemaliza muda wake  na kwamba uongozi wa Chuo utaendelea kupokea ushauri kwa Jaji Mstaafu Samatta pale itakapohitajika.

Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo,Mbeya.

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi