loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barcelona wakubali kukatwa mishahara

BARCELONA wamethibitisha kuwa wameafikiana na wachezaji wao wakatwe mishara yao ili kuokoa  klabu kiasi cha Pauni milioni 109.

Mazungumzo na wachezaji wao juu ya ukatwaji mishahara yamefanyika kwa miezi kadhaa, lengo likiwa ni kuisaidia klabu hiyo inayokabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi kutokana na athari za janga la virusi vya corona.

Kocha wa kikosi hicho, Ronald Koeman amepunguza mshahara wake wa Pauni milioni 10 kwa mwaka wiki hii.

Taarifa ya klabu hiyo inaelezea kwamba ingawa kuna makubaliano kimsingi, wafanyakazi wanaocheza lazima waridhie mapendekezo katika siku zijazo.

Wiki iliyopita mishahara ya Barcelona ilipunguzwa kutoka Pauni milion 601 hadi milioni 342 na La Liga kufuatia shinikizo la kifedha zilizosababishwa na janga la corona.

Rais wa La Liga, Javier Tebas alisema kukatwa kulikuwa muhimu ili kupunguza "matumizi mengi" ya klabu za Hispania, ikizingatiwa kuwa mashabiki bado hawawezi kuhudhuria mechi.

Takwimu za hivi karibuni za Barcelona  zilionesha  kuwa klabu hiyo  ilipata hasara ya Pauni milioni 88 na ilikuwa na deni kubwa, ambalo lilikuwa limeongezeka mara mbili hadi Pauni milioni 440 kufikia Juni 2020.

Barcelona bado wanakubaliana juu ya kupunguzwa kwa mshahara kwa kikosi hicho baada ya wachezaji kukubali kupunguzwa kwa asilimia 70 mnamo Machi.

Wakati wachezaji wengine  kama vile Gerard Pique na Frenkie de Jong - walikuwa wamekubali kurudishwa kwa mshahara kwa asilimia 30, watu wa hali ya juu kama Lionel Messi hawakuwa wamefanya kabla ya Ijumaa.

Marc-Andre ter Stegen na Clement Lenglet pia wamekubaliana kandarasi mpya, ambayo inaonesha wanne wamekubali kupunguzwa mishahara kwa muda mfupi, lakini watalipwa na mpango ulioboreshwa kwa muda mrefu.

Nahodha Messi ndiye anayepata mapato ya juu zaidi klabuni hapo kwa kuwa anaingiza karibu Pauni 500,000 kwa wiki (Pauni milioni 26 kwa mwaka) wakati Antoine Griezmann anachukua karibu Pauni 249,000 kwa wiki (Pauni milioni  15.3 kwa mwaka ) na Philippe Coutinho Pauni 180,000 kwa wiki (Pauni milioni 9.4 kwa mwaka).

KIUNGO wa Manchester City, Kevin de Bruyne atakaa nje ya ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi