loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwanamitondo Marekani aachana na kazi yake

MWANAMITINDO wa Marekani Halima Aden anasema anaacha kazi ya kuwa mwanamitindo kwasababu inaenda kinyume na maadili ya dini yake.

Mwanamitindo huyo, mwenye umri wa miaka 23, amewahi kutangazwa katika majarida ya urembo ya kimataifa kama British Vogue, Vogue Arabia and Allure.

Aden kupitia kwenye mtandao wake wa Instagram, alisema virusi vya janga la corona vimempa fursa ya kufikiria tena kuhusu maadili yake kama mwanamke wa Kiislamu.

 "Kuwa 'Muislamu' ni safari ndefu yenye panda shuka zake ni wakati wangu wakuacha kazi hii na kuangalia fursa nyingine.," alisema.

Akizungumzia kukubali kazi za uanamtindo ambayo inaenda kinyume na maadili ya dini yake, anadai anaweza kujilaumu kwa kujifikiria zaidi kuliko kile hasa kilichokuwa hatarini.

Halima alizaliwa katika kambi ya wakambizi nchini Kenya na wazazi Wasomali kabla ya kuhamia Marekani akiwa na umri wa miaka sita. Alitambuliwa na Shirika la Mitindo la Kimataifa la IMG Models akiwa na umri wa miaka 18 baada ya kushiriki shindano la urembo Marekani la kumtafuta Miss Minnesota, ambako alifika nusu fainali.

Alikuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuvaa hijab katika shindano la urembo na ndani ya kipindi kifupi akawa maarufu kwa mavazi yake ya kipekee katika vipindi maarufu vya fasheni duniani vya kila wiki.

 

BERNARD Morrison ameng’ara baada ya kuifungia timu yake mabao mawili ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi