Australia imeitaka China kuondoa picha bandia inayomwonyesha askari wa nchi hiyo akitekeleza uhalifu nchini Afghanstan jambo lililopelekea uhusiano baina ya nchi hizo mbili kuzorota.
Tayari Waziri Mkuu wa Australia, Scott Morrison amelaani kitendo hicho na kusema kuwa ni cha kuchukiza mno na kutaka picha hiyo iondolewe mara moja mtandaoni.
Picha hiyo, inamwonyesha mwanajeshi wa Australia akiwa ameshikilia kisu chenye damu kwenye koo la mtoto wa Afghanistan, iliwekwa hapo jana kwenye akaunti ya Twitter iliyothibitishwa kuwa ni ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa China, Zhao Lijian.