loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uingereza kuanza matumizi chanjo mpya ya Korona

UINGEREZA imekuwa  taifa la kwanza duniani kuidhinisha matumizi ya chanjo Pfizer/BioNTech kwa ajili ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Korona.

Kwa mujibu wa  Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC),  Mamlaka ya Udhibiti nchini  Uingereza- MHRA imesema chanjo hiyo inayotoa ulinzi wa asilimia 95 dhidi ya Covid-19, ni salama na utaanza kutumika wiki ijayo.

Chanjo hiyo itaanza kutumika siku chache zijazo na makundi ya watu walio hatarini zaidi, wakiwemo wazee, watapewa kipaumbele.

Uingereza imeagiza takribani dozi milioni 40 ambazo zitawatosheleza watu milioni 20, ikiwa mtu mmoja atapatiwa chanjo mara mbili.

Dozi zipatazo milioni 10 zitapatikana hivi karibuni.

Chanjo hii imethibitishwa haraka zaidi kwa matumizi kuliko chanjo nyingine yeyote kwani  imechukua miezi 10 tu chanjo kupitishwa tofauti na awali ambapo ingeweza kuwa zaidi ya miongo kadhaa kupata kibali kabla ya kuanza kutumika.

Licha ya kwamba chanjo itaanza kutumika, bado watu watalazimika kufuata masharti ya kujikinga dhidi ya virusi vya korona, wataalamu wamesema.

Hii ni pamoja na kukaa kwa umbali , kuvaa barakoa na kufanya vipimo .

SERIKALI ya China imesema inatarajia ...

foto
Mwandishi: BBC

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi