loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Urusi kuboresha uwekezaji bidhaa za petroli

RAIS wa Urusi, Vladmir Putin, amesema nchi yake itaweka mazingira bora zaidi ya uwekezaji miradi mikubwa ya vinu vya kuchakata bidhaa mbalimbali zitokanazo na mafuta ya petroli.

Alisema ili kufanikiwa katika miradi hiyo, kuna mambo mawili ya kuzingatia na jambo la kwanza, ni wakati gani mwafaka wa kuanza kazi hiyo na jambo la pili, ni gharama za kazi hiyo ambazo serikali lazima ikabiliane nazo.

Kiongozi huyo aliyasema hayo wakati alipokuwa akifungua mkutano mjini Moscow kuhusu mikakati ya maendeleo katika sekta ya petroli na bidhaa zitokanazo na mafuta hayo yanayotumika zaidi duniani.

“Mamlaka za Urusi zitaendelea kujenga mazingira rafiki kwa ajili ya kuvutia wawekezaji kwa ajili ya kuendeleza taifa letu kiuchumi,” alifafanua Rais Putin aliyeingia Ikulu ya Kremlin, mwaka 1999.

Alisema kupitia vinu hivyo vitakavyojengwa na wakandarasi wa Urusi, taifa hilo litaongeza uwezo wake wa kusafisha mafuta ya petroli ambapo bidhaa kadhaa zitapatikana kwa maendeleo ya Urusi na watu wake.

Kwa mujibu wa Putin, miongozo na taratibu za kiujenzi ambazo zimepitwa na wakati zitaachwa na kutumia mfumo na teknolojia za kisasa zaidi ili kurahisisha uzalishaji utakaokuwa na tija na wa kudumu kwa miaka kadhaa ijayo.

Katika uwekezaji huu, matumizi ya vifaa vya ujenzi vya kisasa pamoja na utumiaji wa teknolojia ya kisasa zaidi maarufu kama ‘teknolojia ya kidijiti’ vinahimizwa sana kutumiwa ili kuwa na miradi ya kisasa na imara zaidi.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi