loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Guterres aonya kuhusu ongezeko la joto duniani

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameikosoa Jumuiya ya Kimataifa kwa kushindwa kupambana na ongezeko la joto duniani na kusema uongozi wa Marekani ni muhimu katika kushughulikia dharura ya mabadiliko ya tabianchi.

Katika hotuba aliyoitoa kwenye Chuo Kikuu cha Colombia, mjini New York, Marekani jana, Guterres ameonya kuwa hali ya sayari ni mbaya na ubinadamu unasababisha vita vya asili.

Alisema viwango vya joto kali, ukame pamoja na bahari kufikia rekodi za juu za joto vinasababishwa na utunzaji mbaya wa mazingira unaofanywa na mwanadamu.

Alitoa mwito wa kutokuweko kwa gesi chafu ya kaboni. Alisema mapambano ya janga la mabadiliko ya tabianchi ni kipaumbele cha juu katika karne ya 21.

“Tunalazimika kuchukua hatua tatu muhimu katika kushughulikia changamoto za hali ya hewa duniani,” alisema Guterres na kuongeza kuwa kuna hatua tatu muhimu za kuchukua.

Hatua ya kwanza kwa mujibu wa Guterres, ni kuteketeza gesi chafu ya kaboni ndani ya miongo mitatu ijayo na hatua ya pili ni kuweka sawa fedha za kimataifa chini ya Mkataba wa Paris.

Guterres alisema hatua ya tatu ni kuilinda dunia na hasa watu na nchi zilizoko katika hatari zaidi kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Alisema ni vigumu kulishughulikia suala la mabadiliko ya tabianchi bila uongozi wa Marekani na kuongeza kuwa makubaliano ya kimataifa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi yasingeweza kufanikiwa bila ushirikiano wa rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama.

Guterres alisema sera za mabadiliko ya tabianchi zimeshindwa kuifikia changamoto hiyo, akibainisha kuwa utoaji wa gesi chafu kwa mwaka 2020 ulikuwa asilimia 60 zaidi kuliko mwaka 1990.

Amesema dunia inaelekea kwenye ongezeko la joto kwa kiasi cha nyuzi joto 3 hadi 5 za Celsius ifikapo mwaka 2100. Mwaka 2019 pia ulishuhudia kiwango cha juu zaidi cha joto la maji ya baharini.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi