loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Iran yakataa masharti ya Biden kuhusu nyuklia

IRAN haitakubali masharti mapya kutoka kwa utawala wa Rais mteule wa Marekani Joe Biden kuhusu mpango wa kinyuklia.

 

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, nchi hiyo imetoa sharti kwa taifa hilo la Marekani kuwa lazima lirudi katika meza ya makubaliano ya 2015 kabla ya mazungumzo kufanyika kuhusu suala hilo.

 

Rais Biden amesema kwamba atairudisha Marekani katika meza ya majadiliano ya mkataba wa kinyuklia na kuondoa vikwazo dhidi ya Tehran itakapofuata makubaliano ya mkataba huo.

 

Pande zote mbili zinaonekana kutaka upande mwingine kufuata masharti ya makubaliano hayo kwanza. Mei mwaka 2018 , Rais wa Marekani Donald Trump alijiondoa katika mkataba huo uliojadiliwa na mtangulizi wake Barrack Obama.

 

Baadaye aliiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi Iran , vikilenga mafuta ya taifa hilo na sekta za kifedha.

 

Iran imepitisha viwango vya mpango wake wa kinyuklia na hivyo kuzua wasiwasi kwamba huenda inatumia mpango huo kama sababu ya kutengeneza bomu la kinyuklia ingawa serikali ya nchi hiyo inasisitiza kuwa lengo la nyuklia hiyo ni la amani.

 

Akihutubia mkutano kupitia mtandao ulioandaliwa na Italia juzi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Javad Zarif alisema kwamba Marekani imekuwa ikikiuka makubaliano ya Umoja wa Mataifa (UN) kwa kuondoka katika makubaliano hayo wakati wa utawala wa Trump alioutaja kuwa 'mbaya' .

 

''Marekani ni inapaswa kukoma kukiuka sheria za Umoja wa Mataifa'' , alisema. Huku waziri Zarrif akisisitiza kuwa Marekani haipo katika nafasi ya kuweka masharti.

 

Biden, ambaye anakaribia kuapishwa kama rais wa 46 wa Marekani Januari 20, mwakani, alisema kwamba atatoa kipaumbele kuirudisha Marekani katika makubaliano hayo na kujaribu kuondoa vikwazo , lakini Iran italazimika kuafiki masharti hayo.

Aliambia gazeti la The New York Times wiki hii kwamba itakuwa vigumu lakini kitu cha mwisho katika eneo hilo ni kujenga uwezo wa kinyuklia .

Wiki iliyopita, Bunge la Iran lilipitisha muswada ambao ungezuia maofisa wa uchunguzi wa UN kuzuru katika kituo chake cha kinyuklia na kuipatia ruhusu serikali kuendelea kujilimbikizia madini ya Uranium hadi asilimia 20 ambayo ni zaidi ya kiwango cha asilimia 3.6 kinachohitajika chini ya makubaliano hayo iwapo vikwazo havitaondolewa katika kipindi cha miezi miwili.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: TEHRAN, Iran

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi