loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dozi ya corona kugharimu Dola 13 Urusi

SERIKALI ya Urusi jana imeanza kutoa chanjo dhidi ya virusi vya corona katika Mji Mkuu wa Moscow kwa kila mwananchi kupata dozi mbili bure.

Taarifa zinasema baadaye dozi hizo zitauzwa kwa Dola za Marekani 26 sawa na Dola za Marekani 13 kwa kila dozi moja. Wizara ya Afya ya Urusi ilisema kiwango hicho kiliwekwa ili kuwawezesha wananchi kumudu gharama za afya.

Ofisa katika Wizara ya Afya, Alexei Kuznetsov, alisema chanjo hiyo Sputnik V itaanza kutumika katika Jiji la Moscow peke yake likiwa na wananchi zaidi ya milioni 11.

“Wizara ya Afya ya Urusi imeamua kuiuza dawa hiyo kwa bei rahisi ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi kuinunua ili kuwakinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona,” ilisema taarifa ya Wizara ya Afya.

Dawa hiyo inatengenezwa na Kituo cha Taifa cha Utafiti wa Dawa cha Gamaleya.  Boksi zima lenye pakiti tano za dozi mbilimbili litauzwa kwa Dola za Marekani 130 sawa na fedha za Kirusi 9,710.

Rais wa Urusi, Vladmir Putin, aliwaomba wananchi wa Urusi hasa katika Jiji la Moscow lenye wakazi zaidi ya milioni 11 kujitokeza kwa wingi kupatiwa chanjo hiyo.

“Dozi hii kwa raia wa Urusi ni bure hivyo wananchi wanaombwa kujitolea ili kuweza kupata dawa hiyo,” alisema Rais Putin katika taarifa yake kwa taifa kupitia Televisheni ya Taifa.

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: MOSCOW, Urusi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi