loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba kujadili sakata la Kichuya

BAADA Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kutangaza kumfungia Kichuya miezi sita au Simba ilipe faini ya zaidi ya Sh. Milioni 290 ili kumnusuru kwa kosa hilo uongozi wa Simba umewataka mashabiki na wanachama wake kuwa wavumilivu wakati wakilishughulikia.

Kichuya ambaye kwa sasa anacheza Namungo, inadaiwa hana kibali cha uhamisho wa kimataifa kutoka klabu ya Ennpi ya Misri, alikokuwa anacheza kwa mkopo akitokea Simba ambako aliondoka bila taarifa kwa viongozi wa klabu hiyo. Akizungumza jana Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda alisema suala hilo litajadiliwa na bodi ya klabu hiyo na baadaye kutolewa maamuzi.

“Tutawafahamisha wanachama wetu kama suala hilo lipo kweli kwani ndio yenye maamuzi kuhusu klabu na siyo mtu mmoja mmoja. Tunaomba wanachama wetu wawe wavumilivu,”alisema Kaduguda.

Alisema lazima wajadiliane kujua nini cha kufanya kwani wanaweza kufanya makosa na suala hilo likarudiwa kusikilizwa na maamuzi yakatenguliwa.

“Pengine umeangushiwa dhahama ambayo sio ya kwako unapotoa maelezo ya kina mnaweza kufikiriwa, hebu tuwe wavumilivu,” alisema.

Naye msemaji wa Namungo, Kindamba Namlia alisema wamepokea suala hilo kwa mshtuko kwani walimsajili Kichuya kama mchezaji huru na amekuwa ni mtu anayeisaidia timu hiyo.

Namlia alisema wanatafuta ushauri wa kisheria juu ya suala hilo wajue wanafanyeje. Kwa mujibu wa Fifa endapo Simba itashindwa kulipa faini hiyo na Kichuya akatumikia adhabu ya miezi sita, inaweza kufungiwa kusajili kipindi cha miaka mitatu.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi