loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Alliance, Yanga vinara Ligi Kuu ya wanawake

TIMU ya Alliance Girls inaongoza ligi ya soka ya wanawake Tanzania Bara ikiwa na pointi tisa baada ya kuifunga Mapinduzi Queens kwa mabao 6-0 katika mchezo wa raundi ya tatu uliofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana Mwanza.

Nayo Yanga Princess wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi sawa na vinara Alliance ila wanatofautiana kwa mabao ya kufunga baada ya kuifunga Mlandizi Queens kwa mabao 2-0.

Simba Queens wanashika nafasi ya tatu kwa pointi saba baada ya kuifunga JKT Queens kwa mabao 3-0 na JKT inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi sita.

Ruvuna Queens wanashika nafasi ya tano wana pointi sita baada ya kuifunga TSC Queens kwa bao 1-0 na Mlandizi Queens wana pointi nne sawa na TSC Queens ambayo inashika nafasi ya saba.

Tanzanite Queens ambayo iliifunga ES Unyanyembe kwa mabao 5-0 inashika nafasi ya nane kwa pointi tatu sawa na Baobab Queens ambayo iliifunga Kigoma Sisterz kwa mabao 2-0 na Kigoma Sisterz ina pointi moja katika nafasi ya 10.

Wageni kwenye ligi ES Unyanyembe na Mapinduzi Queens hawana pointi kwenye michezo yote mitatu waliyocheza katika ligi hiyo inayoshirikisha timu 12.

Wachezaji wa Alliance, Aisha Juma na Kasnath Linus wanaongoza kwa ufungaji wa mabao na wamefunga mabao manne, Oppah Clement wa Simba na Jamila Rajabu wa Baobab wamefunga mabao wawili kila mmoja.

Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea keshokutwa kwa michezo sita kuchezwa kwenye viwanja tofauti

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi