loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Odemba aanza kutoa ‘madili’ ya kimataifa kwa warembo Tanzania

MWANAMITINDO wa Kimataifa wa Tanzania, Miriam Odemba kupitia Kampuni yake ya Miriam Odemba Model Search amefanikisha kupatikana mkataba wa kazi ya mitindo kwa mlimbwende Jasinta Makwabe (25).


Akizungumza na kwa njia simu kutoka Cape Town, Miriam amesema mkataba huo ni wa miaka miwili kati ya mlimbwende huyo na Kampuni ya Ice Models Management iliopo Cape Town, Afrika Kusini na kwamba hiyo ni hatua kubwa kwa taasisi yake ya kuibua vipaji vya ulimbwende iliyopo Tanzania.


Miriam amesema amefurahishwa na hatua ya mlimbwende wake kupata nafasi hiyo nzuri ambayo inadhihirisha kwamba sanaa ya urembo inalipa."Mkataba tayari umesainiwa kwa usimamizi wangu.

Mkataba tayari umesainiwa kwa usimamizi wangu. Haya ni nimafanikio na mwanga makubwa kwangu na matumaini kwa wasichana wenye ndoto za kuwa wanamitindo," amesema.

Amesema, "Nimepata faraja kubwa sana… Nashukuru nipo hapa pamoja na mwanamitindo mwenzangu Fideline Iranga kama mama mlezi wa Jasinta na kila kitu kinakwenda sawa.”

Miriam Odemba amekuwa mwanamitindo aliyeamua kuibua vipaji vya wasichana katika sanaa ya ulimbwende na mtindo ambapo mpaka sasa, mbali na Jasinta ameshawaibua Queen Mugesi, Gihan pamoja na Nelly.

Mbali na kulamba mkataba mnono nchini Afrika kusini, mrembo Jasinta ni mmoja wa walimbwende watakaoshiriki kwenye shindano la kumtafuta mlimbwende wa Afrika linalojulikana kama Miss Africa Calabar linalotarajiwa kufanyika Desemba 29 mwaka huu nchini Nigeria.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi