loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kocha Mwadui: Yanga hainisumbui

KOCHA wa Mwadui FC, Khalid Adam amesema mchezo wa timu yake dhidi ya Yanga  haumuumizi kichwa kwani wachezaji wake wanapokutana na timu kubwa wanajitoa kwa nguvu zote kupata ushindi.

Kocha huyo ametoa kauli hiyo ikiwa imebaki siku moja kabla ya kikosi chake kucheza na Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Kambarage,  Shinyanga.

Adam alisema licha ya kupoteza michezo mitano mfululizo si kigezo cha kupoteza mchezo dhidi ya Yanga kwani wachezaji wake kwenye mechi kubwa wanakuwa vizuri kisaikolojia.

“Siwezi kuwaza kuangaika ni mbinu gani nitakazowapa wachezaji kwenye mchezo huo kwani wanapocheza na timu kubwa wenyewe wanatamani kucheza na timu za aina hiyo na kila mmoja anapenda apangwe kwani wanapata nafasi ya kujitangaza, lakini pia wanakutana na wachezaji wenye uwezo na kila mmoja anaonesha uwezo wake,” alisema.

Adam alisema wanapocheza na  timu za kawaida benchi la ufundi linapata shida kuwaandaa wachezaji kwani wanakwenda kucheza na kikosi cha wachezaji ambao hawana majina lakini pia hawapati nafasi kubwa ya kuwaangalia.

Hata hivyo, alisema mwenendo wa kupata matokeo mabaya bado unamfanya afikirie upya kuangalia wachezaji wengine  watakaongeza nguvu kipindi cha dirisha dogo litakapofunguliwa kuanzia Desemba 15.

Mwadui inashika nafasi ya pili kutoka mwishoni mwa msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 14 wakijisanyia pointi 10, imeshinda michezo mitatu, sare moja na kupoteza mechi 10.

Wakati huo huo Yanga iliondoka Dar es Salaam jana kwenda Shinyanga kwa ajili ya mchezo huo.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema wachezaji 24 na viongozi 10 walitarajiwa kutua Shinyanga jana.

Yanga imecheza michezo 14 na kati ya hiyo imeshinda 10 na kupata sare nne ikijikita katika uongozi wa ligi kwa pointi 34.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi