loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ushindi wampa jeuri Sven

KOCHA wa Simba, Sven Vandenbroeck ameridhishwa na ushindi wa mabao 2-0 walioupata katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam juzi.

Amesema sasa wanajipanga na safari ya kwenda Mbeya  kuwakabili Mbeya City mchezo unaotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Sokoine keshokutwa.

Akizungumza baada ya mchezo wa juzi, Sven alisema wachezaji wake walifanya kazi nzuri na matokeo waliyoyapata yatawasaidia kuwajenga kisaikolijia kujipanga dhidi ya Mbeya City mchezo anaoamini utakuwa mgumu.

“Wachezaji wangu wamefanya kazi nzuri ingawa kuna wengine wanaweza kudharau. Sio siku zote unaweza kuwa kwenye kiwango bora na  kuna mchezo unaweza kupata ushindi wa mabao mengi na mwingine mnaweza msiwe kwenye ubora mkapata ushindi usio mnono, nawapongeza wachezaji wote wamejituma,” alisema Sven.

Pia alimpongeza Mzamiri Yassin kwa kucheza vizuri katika kubaka japo kuna wakati alikosea pasi kadhaa.

“Muda mwingine lazima utegemee hilo sababu anafanya kazi nyingine kwenye timu ambayo ni muhimu zaidi,” alisema.

 

Sven alisema katika mchezo huo licha ya kupata ushindi huo walitengeneza nafasi nyingi ambazo kama sehemu ya ushambuliaji wangeongeza umakini wangeondoka na ushindi wa mabao mengi.

Alisema kwenye mchezo huo alifanya mabadiliko ya kikosi lengo ni kuanza kuandaa miili iwe tayari kwani wana ratiba ngumu kwa mashindano mbalimbali ikiwamo Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Mapinduzi.

“Kwa kuwa tuna kikosi kikubwa ni wakati wa kuanza kufanya mzunguko kwa kumpatia nafasi ya kucheza kila mchezaji ili kuandaa mazingira ya kwenda kukabiliana na ratiba za mashindano mengine mbeleni,” alisema Sven.

Naye kocha wa Polisi Tanzania, Malale Hamsini alikubali matokeo na kusema kikosi chake hakina wachezaji wazuri wa  kumaliza mchezo ndiyo maana walipoteza.

“Simba tuliwakamata kipindi cha kwanza, tulitawala mchezo na tulikuwa tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini kikosi changu sina wachezaji wa kufunga mabao,” alisema.

Alisema baada ya mchezo huo anakwenda kujipanga kwa mchezo dhidi ya Ruvu Shooting na wamepania kupata ushindi.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi