loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yawania rekodi ugenini

VINARA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara Yanga, leo wanashuka dimbani kuivaa Mwadui katika mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Msimu uliopita Yanga ilivuna pointi nne kwa Mwadui baada ya mchezo wa ugenini  kushinda bao 1-0 na wa nyumbani  kupata sare ya bao 1-1.

Timu hizo zinakutana zikiwa katika viwango tofauti, Yanga inashika nafasi ya kwanza kwa pointi 34 baada ya kucheza michezo 14 na kati ya hiyo kushinda 10 na kutoka sare nne ikiwa haijapoteza mchezo.

Yanga imekuwa katika ubora wa hali ya juu ikionesha wazi kuwa haitaki mchezo kwenye mbio za ubingwa baada ya kukosa taji misimu mitatu mfululizo.

Ina kikosi kizuri kinachojituma kuanzia kwenye safu ya ulinzi iliyofungwa mabao matano tu hadi ushambuliaji ingawa hawafungi mabao mengi ila wamekuwa wakipamabana kama sio kuondoka na pointi tatu basi angalau moja.

Yanga imekuwa na rekodi nzuri ya mechi za ugenini  ambapo katika michezo karibu sita waliocheza msimu huu hawajapoteza zaidi ya kutoka suluhu mmoja dhidi ya Gwambina.

Mwadui iko katika wakati mgumu kwa kushindwa kufanya vizuri baadhi ya mechi zake zilizopita ikishika nafasi ya pili kutoka mwisho ikicheza michezo 14, ikishinda mitatu, sare moja na kupoteza 10 ikiwa na pointi 10.

Ni timu itakayocheza kwa presha kuhitaji matokeo mazuri ili kujiondoa hatarini.

Mchezo hautakuwa rahisi kwa kila mmoja Yanga ni muhimu pia kwao kushinda kujiimarisha kileleni kwani wakipoteza au kupata sare watajiweka kwenye presha zaidi kutokana na kasi ya wapinzani wake hasa Simba anayekuja kwa kasi.

Kocha wa Yanga Cedric Kaze alisema wao hawaangalii msimamo wa ligi wanachotaka ni kupata pointi tatu kwa kila mchezo.

“Mwadui iliwahi kuwafunga Simba katika mchezo wa ufunguzi, tunajua hautakuwa mchezo rahisi kwetu ila tumejiandaa vizuri kwa kuzingatia na umuhimu wa mechi na lengo letu ni kupambana kupata pointi tatu,”alisema.

Kwa upande wa Kocha wa Mwadui Khalid Adam alisema Yanga haimuuzi kichwa ameaandaa wachezaji wake vizuri anaamini  watapata matokeo mazuri.

“Ni kweli mwenendo wetu sio mzuri katika ligi ila hatujakata tamaa bado tupo tumejipanga dhidi ya Yanga na naamini tutashinda,”alisema.

Michezo mingine itakayochezwa ni Dodoma Jiji dhidi ya Gwambina kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma na Polisi Tanzania dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Ushirika Moshi.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi