loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba,Yanga wanawake kazi kazi

LEO timu za wanawake za Simba Queens na Yanga Princess zinatarajiwa kutoana jasho katika mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake itakayochezwa uwanja wa Mo Arena Bunju.

Makocha wa timu hizo, Mussa Mgosi wa Simba na Edna Lema wa Yanga kwa nyakati tofauti wametambiana kila mmoja akidai kuwa na uwezo wa kushinda mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka la wanawake nchini.

Mgosi alisema licha ya kuwa nyuma kwa idadi ya pointi bado sio kigezo cha wao kupoteza mechi hiyo.

 “Tumejipanga kuibuka na ushindi kuendeleza historia yetu ya kupata matokeo mazuri dhidi yao, najua mchezo utakuwa mgumu kwakuwa wanatamba wamefanya usajili mkubwa na sisi tumejipanga hawawezi kutuzuia labda watuambie wanakuja kupunguza idadi ya mabao,”alisema Mgosi.

Naye kocha wa Yanga Princess Edna alisema toka msimu uliopita aliwaahidi mashabiki wanatajipanga kuhakikisha wanafuta uteja wa kufungwa dhidi ya watani wao mara kwa mara jambo ambalo wameshalifanyia kazi kwa kusajili wachezaji wenye hadhi.

Msimu uliopita Yanga ilipoteza mechi zote mbili kwa mtani wake.

“Tunakikosi ambacho kinaushindani na kama mnavyoona tumeshinda michezo yetu yote na tunahakikisha tunaenda kupata ushindi dhidi ya watani wetu kurudisha furaha iliyopotea baada ya kufungwa kwenye michezo iliyopita.

“Safari hii tumejipanga kubeba ubingwa na ilitutimize malengo lazima kila mchezo tupate pointi tatu,”alisema Edna.

Yanga ndio kinara wa ligi hiyo ikiwa na pointi tisa na Alliance iliyo nafasi ya pili na Simba ni ya tatu ikiwa na pointi saba.

Timu hizo zinaingia kwenye mchezo huo huku Simba wakiwa na rekodi nzuri  msimu uliopita ikivuna pointi sita katika mechi zote mbili dhidi ya Yanga kwa ushindi wa mabao 5-1 katika mechi ya kwanza kabla ya kushinda 3-0 mechi ya pili.

MBIO ya Tanzania Women ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi