loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Zuchu ashukuru mashabiki wake

BAADA ya kuchaguliwa  kuwania tuzo za MTV, MAMA Award 2021, msanii wa kizazi kipya, Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ amewashukuru watanzania kwa kuendelea kumuunga mkono.

Zuchu ametoa kauli hiyo jana ikiwa siku moja tangu jina lake kutangazwa na waandaji wa tuzo hizo Uganda kama  miongoni wa wasanii wanaowania kipengele cha wanamuziki waliopata mafanikio kwa muda mfupi.

Akizungumza Dar es Salaam jana  Zuchu alisema amefurahi  kupata nafasi hiyo kwa kuiwakilisha nchi kwenye tuzo hizo na kwamba anathamini mchango wa watanzania wote kwa kumfanya aonekane na waandaaji hao .

“Nashukuru kwa kupata nafasi hii ya kuiwakilisha nchi kwenye tuzo za  MAMA Award 2021 baada ya kurudishwa lakini pongezi kubwa nazirudisha kwa watanzania wanaoniunga mkono kwa kazi zangu kuonekana na waandaaji wameniona,”alisema Zuchu.

Kwenye mashindano hayo Zuchu amepangwa katika kipengele cha ‘Best Breakthrough Act’anakabiliwa ushindani kutoka kwa Elaine na  Focalistic wa Afrika Kusini, Tems na Omah Lay  wote kutoka Nigeria, John Blaq (Uganda) na Sha Sha (Zimbabwe).

Mbali na Zuchu wasanii wengine wanne  wanaotarajiwa  kuiwakilisha nchi kwenye tuzo hizo zilizopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka ujao ni Naseeb Abdul ‘Diamond’ Rajab Kahali ‘Harmonize’ kundi la Rostam linaloundwa na Boniventure Kabongo ‘Stamina’ na Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’wakiwa wamepangwa vipengele tofauti. 

KIWANGO kizuri ilichoonesha Simba katika mchezo ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

1 Comments

  • avatar
    Leon Mwandja
    17/12/2020

    mutambue kwamba sio tanzanien tuh ndo inawapaga sapoti kunazingine inchi ambao zina wapa sapoti bila nyinyi kujijua

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi