loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga yaisambaratisha Mwadui 5-0, Yacouba mwiba

YANGA imeendelea kujikita kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuifunga Mwadui 5-0 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa CCM Kambarage, mjini Shinyanga leo jioni. 

Dalili za Yanga kushinda kwa idadi kubwa ya mabao zilianza kuonekana tangu kipindi cha kwanza baada ya Deus Kaseke kutikisa nyavu za wenyeji katika dakika ya sita tu ya mchezo huku Yacouba Sogene aliyekuwa anaisumbua ngome ya wapinzani akifunga goli la pili dakika nane baadaye.

Timu hizo zilikwenda mapunziko huku Yanga ikiongoza kwa mabao hayo mawili.

Hata hivyo, takribani dakika nne tu tangu kuanza kwa kipindi cha pili, Yacouba aliyekuwa kwenye kiwango cha juu cha mchezo alifunga goli la pili huku Tuisila Kisinda na nahodha Lamine Moro wakifunga goli moja kila mmoja katika dakika za 56 na 70.

Kwa matokeo hayo, Yanga imejichimbia kileleni ikiwa imekwishajikusanyia jumla ya pointi 37 baada ya kucheza michezo  15.

Simba ambayo ina viporo vya ligi kutokana na ushiriki wake kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itashuka katika uwanja wa Sokoine kesho, Jumapili, kumenyana na wenyeji Mbeya City.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi