loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga ya mabao yatesa

TIMU ya Yanga imeendeleza raha kwa mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga jana.

Mabao mawili yalifungwa na Yacouba Songne, Deus Kaseke, Tuisila Kisinda na Lamine Moro.

Huo ni ushindi wa kwanza mkubwa kwa Yanga msimu huu baada ya ule wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union huku nyingine wakishinda kati ya bao moja au mawili.

Kwa ushindi huo Yanga inaendelea kujikita kileleni mwa ligi kwa kufikisha pointi 37 katika michezo 15, ikifuatiwa na Azam FC yenye pointi 27 katika michezo 14 na Simba pointi 26 baada ya kucheza michezo 12.

Awali Yanga ilianza mchezo huo kwa kasi na kupata bao la uongozi lililofungwa na Kaseke dakika ya 6 baada ya pasi nzuri ya Songne ambaye naye pia alifunga bao la pili na la tatu dakika ya 14 na 49.

Kabla ya Songne kufunga bao la tatu, timu hiyo ilikwenda mapumziko ikiwa mbele mabao 2-0 na kuongoza katika umiliki wa mpira.

Kipindi cha pili ilirudi kwa kasi tena na mshambuliaji huyo kufunga bao hilo kisha dakika ya 57 Kisinda naye akafungua bao la nne akimalizia pasi ya Songne.

Yanga hawakuridhika, waliendelea kufanya mashambulizi na dakika 69 walipata bao la tano lililofungwa na Lamine Moro akimalizia krosi ya Farid Mussa aliyeingia dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Songne.

Timu hiyo ilikuwa na uwezo wa kuondoka na mabao zaidi kutokana na kutengeneza nafasi nyingi ila walishindwa kuzitumia.

sMwadui ilitengeneza nafasi kama mbili lakini walikosa umakini katika umaliziaji. Timu hii bado hali siyo shwari kwani huo ni mchezo wa tano mfululizo inapoteza ikiwa inashika nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na pointi 10.

MCHEZO wa Ligi Kuu ya Soka la Wanawake kati ya ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi