loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Gulam, Bayi warejea kwa kishindo TOC

RAIS na Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Gulam Rashid na Filbart Bayi wameshinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa kamati hiyo uliofanyika Dodoma.

Kati ya kura 35 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano huo,  Rashid na Bayi kila mmoja alipata kura za ndio 34 ikiwa ni sawa na asilima 97.14 ya kura zote halali zilizopigwa.

Nafasi hizo za Bayi na Gulam hazikuwa na wapinzani pamoja na zile za katibu msaidizi, mhazini mkuu na msaidizi wake, wakati ya Makamu wa Rais ndio ilikuwa na wagombea  wawili, Henry Tandau na Muharam Mchume.

Akitangaza motokeo hayo karibu saa 6:00 usiku wa kuamkia jana Mwenyekiti wa  Kamisheni ya Uchaguzi ya TOC, Llyod Nchunga alisema aliyekuwa makamu wa rais wa TOC kabla ya uchaguzi huo, Tandau alimbwaga vibaya mpinzani wake katika nafasi  hiyo kwa kupata kura 30 kati ya 35 zilizopigwa.

Alisema ushindi huo ni sawa na asilimia 88.71, wakati Mchume aliyetamba kuchukua kiti hicho aliambulia kura tatu mbazo ni sawa na asilimia 8.57, huku Suleiman Jabir ikishinda kiti cha ukatibu msadizi baada ya kujipatia kura za ndio 34 ambazo ni sawa na asilimia 97.124.

Charles Nyange anaendelea kuwa mhazini mkuu baada ya kupata kura 31 ambazo ni sawa na asilimia  88.57, wakati Zaidy ameendelea kuwa mhazini msaidizi baada ya kupata kura zote za ndio.

Wajumbe kutoka Tanzania Bara waliopita na idadi ya kura walizopata zikiwa katika mabano ni Noorelain Shariff (21), Irene Mwasanga na mjumbe mpya Suma Mwaitenda ambao kila mmoja alipata kura 17.

Wajumbe ambao kura zao hazikutosha ni Donath Massawe (14), Devotha Marwa (11), Amina Lyamaiga (7), Suleiman Nyambui (6) na Juma Jamby (3).

Wajumbe kutoka Zanzibar waliopita ni Makame Machano (33), Nasra Mohamed (28) na Seleman Ame (19).

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi