loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Serengeti Boys kuivaa Rwanda leo

KIKOSI cha timu ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti boys, leo kitakuwa na kibarua kizito kitakapomenyana na wenyeji Rwanda kwenye mechi ya michuano ya Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.

Michuano hiyo inafanyika chini ya usimamizi wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na mechi ya Serengeti na wenyeji itachezwa kwenye uwanja wa Rubavu Rwanda.

Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa juzi lakini uliahirishwa kutokana na waamuzi kushindwa kufanyiwa vipimo vya corona na hivyo walilazimika kuwekwa karantini kabla ya kuruhusiwa kuchezesha mechi hiyo.

Serengeti Boys imepangwa kundi B pamoja na timu za Rwanda na Djibouti. Timu zitakazocheza fainali zitafuzu moja kwa moja michuano ya Afrika, Afcon.

Akizungumzia mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Hababuu Ali alisema wachezaji wake wapo vizuri toka juzi walikuwa wanafanya mazoezi kwenye uwanja wa Gesenyi.

“Wachezaji wangu wote wapo tayari ingawa hakuna mchezo rahisi, tumejipanga kuibuka na ushindi kwani tunaingia na kaulimbiu ya kwenda kushiriki fainali za mataifa Afrika (Afcon),” alisema.

Alisema kutokana na kufuata kanuni za kujikinga na corona imekuwa changamoto kupata mipango ya wapinzani pamoja na taarifa zao.

“Najua watakuwa wanafanya mazoezi kwakuwa wao ni wenyeji lazima watahitaji kubakisha kombe lakini na kikosi changu ndoto yetu ni Afcon tunapambana tupate ushindi,” alisema.

Alisema kikosi chake kinaundwa na wachezaji 23 na wote amewapa mbinu ya kumaliza mchezo mapema kwa kufunga mabao ili  kuwachanganya wapinzani.

Alisema kikosi hicho kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea kwenye michuano hiyo ikiwamo kwenda kuweka kambi  ya wiki mbili Morocco ambako walicheza michezo miwili ya kirafiki kama sehemu ya kuwaanda wachezaji kisaikolojia.

Michuano hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Desemba 22.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi