loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kenya yaanza kwa sare Cecafa

TIMU ya vijana ya Kenya chini ya umri wa miaka 17 imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Ethiopia kwenye mechi ya michuano ya Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Kenya ilipata mabao yake kupitia kwa James Gachago na Khamis Nyale huku mabao ya Ethiopia yakifungwa na Bereket Jiru na Miraj Nagash.

Kenya ilianza mechi kwa kasi ikitafuta bao la mapema na dakika ya 13 wakapata bao la kuongoza kupitia kwa Gachago.

Bao hilo lilidumu mpaka mapumziko.

Ethiopia walikuwa bora zaidi kipindi cha pili wakisaka bao la kusawazisha.

Jitihada zao zilizaa matunda na kupata bao dakika ya 60 kupitia kwa Jiru aliyetumia vema makosa ya safu ya ulinzi ya Kenya na kuandika bao hilo la kusawazisha. 

Dakika ya 86, Nyale alifunga bao la pili kwa Kenya na kuonekana kama lilikuwa la ushindi, lakini wapinzani wao hawakukata tamaa. 

Zikiwa zimesalia dakika mbili mechi kumalizika Nagash alifunga bao la pili na kuihakikishia timu yake kugawana pointi. 

Kenya sasa itacheza na bingwa mtetezi Uganda kesho. 

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ...

foto
Mwandishi: RUBAVU, Rwanda

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi