loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

 Vigogo 22 TRA wasimamishwa kwa tuhuma za ufisadi, uzembe

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk Edwin Mhede kuwasimamisha kazi watumishi 22 wa mamlaka hiyo wakiwemo baadhi ya Maneja wa TRA wa Mikoa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili za kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kujihusha na vitendo vya kifisadi na uzembe kazini.

Dkt Mpango ametoa maagizo hayo jijini Dodoma, alipokutana katika Kikao Kazi na Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Mameneja wa mikoa wa Mamlaka hiyo, kupanga mikakati namna ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini pamoja na kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato ya kodi na maduhuli ya Serikali.

Aliagiza uchunguzi wa kina ufanyike kwa watumishi hao wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya rushwa, kutosimamia ipasavyo matumizi ya mashine za kutolea stakabadhi (EFD), kuwabambikia kodi kubwa wafanyabiashara na kuagiza apatiwe taarifa ya utekelezaji wa maelekezo yake ndani ya siku 90 kuanzia leo.

Waliotakiwa kusimamishwa ni: Tanga: Ofisa wa TRA Brighton Kasilo, Rukwa: Kaimu Meneja Nkasi Rogers Mkama, Shinyanga: Meneja wa kitengo cha ukaguzi Sara Senso na Meneja wa EFD Kwibin Nyamuhanga, Dodoma: Meneja wa Mkoam, Kabula Mwemezi, Kigoma: Meneja wa Mkoa Jacob Mtemang'ombe, Kasulu: Meneja wa TRA Benward Mwakatundu, Songwe: Ofisa TRA Janeth Mlack, na Joshua Daudi Samwel,

Wengine ni Kilimanjaro: Msimamizi wa kituo cha Tarakea, Maududi Tingwa, Same: Adam Benta na Adam Ruhusa, Njombe: Maofisa Hilda Samuel Mahenge, Ibrahim Lyndama na Geofrey Mwinuka, Kagera: Meneja Biharamulo Alex Chacha, Ilala: Maofisa Stephen Kauzen, Kimweli, Ngobya, Raphael Meng'alai, Benedict Kasele na Nicodemus Mwandago, na Lindi: Kaimu Meneja Ruangwa, Florian Rubambwa.

“Nakuagiza Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede uwapumzishe kazi (relieve them from duty) kuanzia leo kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka 2003 na umwagize Mkuu wa Idara ya Mambo ya Ndani (internal Affairs) awachunguze wahusika wote ndani ya siku 90 na nipatiwe nakala ya taarifa hiyo ya uchunguzi na hatua zilizochukuliwa dhidi ya kila mmoja wao," alisema Dkt Mpango

Vilevile, Dkt Mpango alimwagiza Kamishna Mkuu wa TRA kufanya uhamisho wa lazima wa Maofisa waliokaa muda mrefu katika kituo kimoja cha kazi na kwamba anatambua zoezi hilo litagharimu fedha nyingi lakini ni bora kufanya uhamisho wa watumishi hao kwa kuwa kukaa kwao muda mrefu kwenye vituo vyao kuna athiri utendaji kwa kuwa wengi wao wana mitandao ya kuiba fedha za umma.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Maalum, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi