loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Takukuru yarejesha mil 5.4/- za mwalimu aliyetapeliwa na QNet

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Geita imefanikiwa kurejesha zaidi ya Sh milioni 5.4 kwa mwalimu Rose Mgimba wa Shule ya Msingi Lukaranga iliyopo Halmashauri ya mji wa Geita aliyekuwa ametapeliwa na kampuni inayofanya biashara za mtandaoni ya QNET.

Akitoa taarifa hiyo jana, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita, Leonidas Felix alisema hatua hiyo inafuatia baada ya ofisi yake kupokea na kufanyia uchunguzi malalamiko kutoka kwa mwalimu huyo akidai kutapeliwa na QNet kiasi hicho cha fedha kwa njia ya ushawishi, kurubuniwa na kuahidiwa kutengeneza fedha mara dufu baada ya kuwezeshwa kufungua duka mtandaoni.

Leonidas alisema kutokana na uchunguzi uliofanyika dhidi ya malalamiko hayo imebainika kuwa kampuni hiyo ya QNet inaendesha biashara hiyo bubu mkoani Geita kwa kuwatumia watu wanaojiita wawakilishi huru ambao ndio wanaoshawishi na kuwalaghai watu kujiunga katika mtandao wa biashara hiyo.

Alisema uchunguzi umeonyesha kampuni ya QNET haijasajiliwa na msajili wa makampuni kufanya biashara na haina leseni ya biashara ambapo kiongozi wa wawakilishi wa kampuni hiyo Geita aitwaye Aneth Bikombo amekuwa akifanya biashara hiyo kupitia kivuli cha Taasisi yake isiyokuwa ya Kiserikali (NGO) iliyosajiliwa kwa jina la Teknolojia katika maendeleo endelevu (Technologies In Sustainable Development Organization).

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha zake, Mwalimu Rose alisema alishawishika kujiunga na mtandao wa QNet na kukubali kutoa fedha hizo baada ya kuahidiwa kufunguliwa duka mtandaoni na mwisho wa siku aliletewa bidhaa ambazo aliambiwa ni kwa matumizi yake ya nyumbani na siyo duka.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Geita

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi