loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usafiri mikoani wadorora Ubungo

KUCHELEWA kufungwa kwa shule, kumechangia kuiathiri sekta ya usafiri wa mabasi, hususani katika kipindi hiki cha mwisho wa mwaka kutokana na mabasi mengi kusafiri na abiria wachache, ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Akizungumza na HabariLEO jana, Naibu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), John Mbazi alisema hali hiyo imesababisha uwepo wa idadi ndogo ya abiria  hususani wanaosafiri kutumia Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo (UBT).

“Ukweli ni kwamba kuchelewa kufungwa kwa shule mara baada ya utaratibu wa Wizara ya Elimu tangu kumalizika kwa ugonjwa wa Covid 19, kumesababisha kupungua kwa idadi ya abiria, hii inatokana na kuwa wazazi wengi hawawezi kusafiri bila watoto wao,”alisema.

Alisema matarajio yao hali hiyo kituoni inaweza kubadilika kuanzia wiki ijayo mara baada ya shule mbalimbali kufungwa kuanzia kesho, jambo linaloweza kuwafanya wazazi wengi kuanza kupanga safari zao, hivyo kuamsha upya hali ya usafiri kituoni hapo.

Mkuu wa Kitengo cha Habari cha Taboa, Mustafa Mwalongo alisema hadi sasa usafiri  wa mabasi hususani katika kituo hicho cha Ubungo, hauna  changamoto zozote zilizokuwa kipindi kama hiki miaka ya nyuma, kiasi cha kuwafanya watu kupata taabu ya usafiri.

Aidha, alisema kwa kuwa zimesalia siku chake kuelekea sikukuu, matarajio yao huenda hali hiyo itabadilika. Aliwataka wananchi wote wanaotarajia kusafiri kwa ajili ya sikukuu hizo, kukata tiketi zao mapema ili kuepuka usumbufu.

“Ukweli mwaka huu umekuwa wa tofauti sana na huko nyuma, abiria bado ni wachache kiasi cha kusababisha hata baadhi ya mabasi kuamua kusitisha safari zake kwa kukosa abiria, imani yetu pengine hali inaweza kubadilika kuanzia wiki ijayo,”alisema.

Alisema miaka ya nyuma nyakati kama hizi, kituo cha mabasi cha Ubungo na vinginevyo mikoani, hutawaliwa na pilika za abiria wengi kutaka usafiri  kwenda mikoani, hususan mikoa ya Kaskazini, kwa ajili ya kusheherekea na ndugu zao sikukuu za mwisho wa mwaka.

NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

1 Comments

  • avatar
    Lameck Kitinusa
    17/12/2020

    Hakuna cha kuchelewashwa kwa kufungwa shule wala nn Hali ya uchumi imekuwa mbaya tofauti na miaka ya NYUMA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi