loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dodoma Jiji yaipania Yanga

KOCHA Mkuu wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata amesema kikosi chake kinataka ushindi wa pointi tatu dhidi ya Yanga katika mchezo utakaochezwa keshokutwa kwenye Uwanja wa Sheikh Abeid mkoani Arusha.

Akizungumzia mchezo huo jana, Makata alisema tatizo lililokuwa linaikabili timu yake hasa katika michezo ya ugenini amelifanyia kazi hivyo ana amini atapata ushindi katika mchezo ujao dhidi ya timu aliyosema ni bora.

“Tatizo kubwa lilikuwa ni umaliziaji na hilo ninaendelea kulirekebisha kila baada ya mechi. Nimewajenga wachezaji wangu kufanyia kazi mapungufu ya umaliziaji na kuhakikisha wanatumia nafasi zote wanazopata ili katika michezo ijao tufanye vizuri zaidi,” alisema.

Kocha huyo wa zamani wa Alliance, Tanzania Prisons na JKT Oljoro ameiwezesha Dodoma Jiji kushinda michezi mitano, sare nne na kupoteza mitano ikiwa katika nafasi ya tisa kwa pointi 19 katika  michezo 14 iliyocheza.

Timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu ilianza ligi vizuri,  lakini kadiri siku zinavyokwenda imekuwa ikipanda na kushuka nafasi za katikati kutokana na upinzani mkali inaopata.

Dodoma Jiji itakutana na Yanga iliyoko katika uongozi wa ligi kwa pointi 37 baada ya kucheza michezo 15, kushinda 11, sare nne ikiwa haijapoteza mchezo wowote.

KIWANGO kizuri ilichoonesha Simba katika mchezo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi